Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Machi 10, 2020 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya uamuzi ufuatao;

Ligi Kuu ya Vodacom:

Mechi namba 253: Mwadui FC 2 v Police Tanzania FC 1

Kocha Msaidizi wa Police Tanzania, Ally Mtuli anapelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kumshambulia mwamuzi msaidizi Neema Mwambashi na kumtolea matusi ya nguoni.

Mechi hiyo ilichezwa Machi 04, 2020 katika Uwanja wa Mwadui FC mjini Shinyanga.

Mechi namba 268: Lipuli Fc 3 vs Ndanda Fc 3

Mchezaji wa Klabu ya Lipuli Fc Seif Ng’ingo na Mchezaji wa Klabu ya Ndanda Abubakar Hashimu wamepigwa Faini ya kiasi cha Tsh.500,000/=(Laki tano)Kila mmoja na kufungiwa Mechi tatu kwa kosa la kufanya vitendo vyenye kuashiria imani za ushirikina na uchawi hadharani, katika mechi iliyochezwa Machi 04,2020 katika uwanja wa Samora Mkoani Iringa.

Adhabu hii imetolewa kwa mujibu wa Kanuni namba 38(9) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.

Mechi namba 260: Azam FC 2 v Simba SC 3

Klabu ya Simba imepewa Onyo Kali baada ya kuchelewa kufika uwanjani na kufika uwanjani saa 12:45 badala ya saa 12:00. Mechi hiyo ilichezwa Machi 04,2020 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Adhabu hiyo ni kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo

Mechi namba 260: Azam FC 2 VS Simba SC 3

Kocha wa Klabu ya Azam FC Aristica Cioba ametozwa Faini ya kiasi cha Tsh.500,000/=(Laki Tano) kwa kosa la kugoma kuongea na waandishi wa habari mara baada ya mchezo kumalizika.

Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni namba 41(12) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Makocha.

Ligi Daraja la Kwanza:

Mechi namba 95: Dodoma FC 4 VS Pan African FC 1

Klabu ya Dodoma FC imepigwa Faini ya kiasi cha Tsh.500,000/=(Laki Tano) kwa kosa la kutokufungua Mlango Rasmi katika uwanja wao wa nyumbani hali iliyosababisha wachezaji na viongozi wa Pan Afican kutumia mlango usio rasmi wa kuingia Uwanjani katika mechi iliyochezwa Machi 1,2020 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 43(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti kwa Klabu

Mechi namba 98: ​Arusha FC 1 VS Geita FC 1

Klabu ya Geita FC imepigwa Faini ya kiasi cha Tsh.500,000/=(Laki Tano) kwa kosa la kutoingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo muda wa Mapumziko katika mechi iliyochezwa Machi 7,2020 katika uwanja wa Sheik Amri Abeid jijini Arusha.

Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi daraja la kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo.

Mechi namba 102: Dodoma FC 2 VS African Lyon FC 1

Klabu ya Dodoma FC imepigwa Faini ya kiasi cha Tsh.1, 000,000/=(Milioni Moja) kwa kosa la kutokufungua Mlango Rasmi katika uwanja wao wa nyumbani hali iliyosababisha wachezaji na viongozi wa African Lyon kutumia mlango usio rasmi wa kuingia Uwanjani katika mechi iliyochezwa Machi 8,2020 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 43(1) ya Ligi daraja la kwanza kuhusu Udhibiti wa Klabu.

Ligi Daraja la Pili:

Mechi namba 36B: ​Usalama FC 1 VS Kitayosce FC 1

Klabu ya Usalama FC imepigwa Faini ya kiasi cha Tsh.500,000/=(Laki Tano) kwa kosa la Washabiki wake Kufanya vurugu na kumrushia jiwe mwamuzi wa mchezo Jackson Samwel katika mechi iliyochezwa Machi 8,2020 katika uwanja wa Singe Sekondari Mkoani Manyara.

Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 43(1) ya Ligi daraja la Pili kuhusu Udhibiti wa Klabu.

Mechi namba 31C: ​Mtwivila FC 0 VS Tukuyu Star SC 0

Viongozi wa Klabu ya Mtwivila FC, Meneja wa Timu Omary Albert, Katibu wa Timu Oscar Mkusa, Kocha Mkuu Petro Mlope Kwa pamoja wanapelekwa kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kosa la udanganyifu wa Leseni ya mchezaji Christopher Rashid Kidava katika Mechi iliyochezwa Februari 29, 2020 katika uwanja wa Mkwawa Mkoani Iringa,Vilevile Klabu ya Mtwivila FC imepoteza Mchezo huo kwa kosa la kumchezesha Mchezaji ambaye hajasajiliwa .

Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 43(23) ya Ligi daraja la Pili kuhusu udhibiti wa Klabu.Hivyo Klabu ya Tukuyu Star FC imepewa Ushindi wa Pointi tatu na Magoli Matatu kwa uzingativu wa kanuni ya 14(36) ya Ligi daraja la pili Kuhusu taratibu za Mchezo.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.