Timu ya Taifa ya Wanawake U20 “Tanzanite” inatarajia kurudi leo ikitokea Port Elizabeth,Afrika Kusini ilipokua ikishiriki mashindano ya Cosafa.

Tanzanite itatua saa 12 na nusu jioni ikiwa na Kombe la Ubingwa wa mashindano hayo.

Katika mashindano ya Cosafa,Tanzanite kwenye hatua ya makundi ilipata ushindi mechi mbili 2-0 dhidi ya Botswana,8-0 dhidi ya Eswatini na kupoteza mchezo mmoja na Zambia kwa mbaoa 2-1.

Ilipata ushindi nusu fainali dhidi ya Afrika Kusini wa mabao 2-0 kabla ya kuifunga Zambia 2-1 katika mchezo wa fainali iliyochezwa jana Uwanja wa Wolfson.

Mbali na Kombe Tanzanite wamepata medali za dhahabu huku Nahodha Enekia Kasonga akiibuka kuwa mchezaji Bora wa Mashindano.