Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kesho Jumanne Machi 12,2019 litaendesha semina kwa Klabu za Ligi Kuu (TPL).
Semina hiyo ya siku moja itafanyika Hoteli ya DEMAGE,Kinondoni.
Makatibu wa Klabu 20 za Ligi Kuu watahudhuria semina hiyo itakayoanza saa 2 asubuhi.