Makocha Soka la Ufukweni Kunolewa kwa Siku Tano TFF

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF linaendesha kozi ya siku tano maalumu kwa  makocha wa mpira wa miguu soka la ufukweni inayojumuisha makocha mbalimbali kwa lengo la kuwaongezea maarifa yatakayo pelekea manufaa ya mchezo huo ikiwa ni pamoja na kuendana na mabadiliko kulingana na wakati.

kozi hiyo inayo jumuisha washiriki 25 watakao nolewa ipasavyo na mkufunzi wa FIFA kwa upande huo wa soka la ufukweni Talib Hilal ambaye pia ni kocha wa soka hilo huko nchini Oman imeanza rasmi Novemba 11, 2023 ikifunguliwa na mkurugenzi wa Sheria, Habari na Masoko Boniface Wambura.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kozi hiyo Boniface Wambura alisema kuwa TFF imefarijika kupata mkufunzi kutoka FIFA kwaajili ya kuwaendeleza makocha wazawa kwa upande wa soka la ufukweni na kwamba hayo yote yanayofanywa na TFF ni kutokana na mpango mkakati uliopo chini ya Rais Walllace Karia.

“Ni matumaini yetu kuwa baada ya kozi hii tutakwenda kuona mabadiliko makubwa kwenye soka letu hasa kipindi ambacho ligi itarejea ili hata mkufunzi aone matunda ya kile alicho kipanda kwenu” alisema Wambura.

Hata hivyo mkufunzi huyo wa FIFA kutoka Oman Talib Hilal aliwataka washiriki hao waweze kujitoa ipasavyo kwenye kupokea mafunzo hayo ili wote kwa pamoja waweze kufikia malengo waliyojiwekea.

Talib alisema matumaini yake ni makubwa sana kwenye soka la ufukweni hapa nchini, hata amewahi kumuhusisha Rais Karia kuwa anatamani Tanzania ifike kwenye hatua ya kucheza Kombe la dunia katika mashindano hayo.

“Kabla niliwahi kukaa na Rais Karia na nikamuhusisha kuwa natamani kuiona Tanzania ikicheza Kombe la dunia kwani naamini hakuna ugumu kufika hapo kutokana na upatikanaji wa maeneo mengi maalum kwa mchezo huo hapa, hivyo ni kujitoa kwenu ndio kutapelekea kufikia malengo hayo ya TFF ili iwe ni sehemu ya kufungua baraka ya kuendelea kufika kila mwaka” alisema mkufunzi huyo

kozi hiyo ya kuwaendeleza makocha hao itaendelea mpaka Novemba 17, 2023 ikiwa ni kipindi ambacho pia ligi kuu ya soka la ufukweni imesimama baada ya kutamatika kwa raundi 2.