Mashindano ya FIFA Series ni Faida kwa Stars

Kauli ya Mkurugenzi wa Sheria, habari na Masoko TFF Boniface Wambura kufuatia mashindano mapya ” FIFA Series 2024″ yaliyoanzishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA Kwa lengo la kukutanisha timu za mabara tofauti kwenye Michezo ya kirafiki Kwa mujibu wa kalenda ya FIFA maarufu FIFA Week.

Boniface Wambura ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache kabla timu hiyo ya Taifa Stars haijashuka dimbani Kwa mechi zake mbili za kirafiki( FIFA Series ),ambapo Stars inatarajia kucheza na Bulgaria Machi 22 na baadae dhidi ya Mongolia tarehe 25 mwezi Machi mwaka huu.

“Tumekuwa na bahati kati ya timu 20 za kwanza kucheza mechi za mashindano haya mapya, kwetu ni Faida kubwa Kwa wachezaji kupata uzoefu wa kucheza na wachezaji wa mabara tofauti, lakini pia ni nafasi Kwa kocha kusoma kikosi chake ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mashindano makubwa ya Kufuzu Kombe la Dunia na AFCON yaliyo mbele yetu. Matumaini yetu ni kutumia vyema nafasi hii kuweza kufikia hatua kubwa ya malengo ya timu naTaifa Kwa ujumla” alisema Wambura.

Mbali na hayo pia akiwa na timu hiyo wakati wa mazoezi yaliyofanyika uwanja wa Olimpiki wa Baku Rais wa ZFF ambaye ni mkuu wa msafara wa timu ya Taifa Stars Dkt. Suleiman Jabir alisema wachezaji wote wakiwemo wale wanaocheza nje ya Tanzania tayari wamewasili kambini na kuungana na wenzao ambao waliondoka hapa nchini Machi 17, 2024.

Stars inaendelea kujiandaa na mechi hizo mbili ambapo imekuwa ikifanya mazoezi kwenye uwanja wa Olimpiki wa Baku, Azerbaijan tangu Machi 19, 2024.