Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Mechi Mbili za Mwisho Kuamua Nani Kushuka Ligi Kuu NBC Bara!

Michezo mitatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara ilipigwa Juni 22,2023 kwenye viwanja tofauti tofauti huku ligi hiyo ikiwa bado ipo kwenye kitendawili cha timu ipi itakayoshuka daraja na ipi itakwenda kucheza mchezo wa mtoano (Play Off) ili kuzipata timu 16 zitakazo salia kwenye ligi hiyo msimu wa 2022/2023.

Katika michezo mitatu iliyopigwa taraehe 22/06/2022, ni KMC na Mbeya Kwanza (Azam Complex) ambapo Mbeya Kwanza waliambulia kichapo cha mabao 4-1; Magoli 3 wakijifunga wenyewe baada KMC kuwapelekea presha kubwa iliyowalazimisha kufanya makosa na kupoteza mchezo huo. Bao moja linalokamilisha idadi ya mabao manne ya KMC lilifungwa na Matheo Anthony kwa mkwaju wa penati wakati bao la kufutia machozi kwa upande wa Mbeya Kwanza likipachikwa na Habibu Kiyombo.

Mechi nyingine ilikuwa kati ya Young Africans na Polisi Tanzania; mchezo huo ukipigwa majira ya saa 12:30 jioni katika dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam ambapo timu ya Young Africans ilishinda bao 2-0; mabao yaliyopatikana kipindi cha kwanza kupitia Feisal Salum (Fei Toto) na Chiko Ushindi Wakubanza.

Mbali na michezo hiyo miwili, Azam FC nayo iliwaakaribisha Tanzania Prisons manamo majira ya saa 2:30 usiku amabapo Azam ilishinda bao 1-0; Mfungaji wa bao ni Idrisa Mbombo, aliyefunga katika kipindi cha kwanza. Ushindi uliowapandisha kwenye nafasi ya 3 baada ya kufikisha alama 43 wakizipiku alama 42 za Geita Gold baada ya timu hizo kushuka dimbani mara 28 zikibakiwa na michezo miwili kila mmoja.

Kitendawili cha nani atashuka daraja moja kwa moja, na nani atacheza mechi za mtoano kinachagizwa zaidi baada ya timu takribani sita kuwa kwenye uwezekano wa kucheza “Play Off” au kushuka daraja kabisa kutokana na kuwa katika nafasi ya hatari kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ambayo imekuwa na ushindani wa aina yake msimu huu wa 2021/2022 unaoelekea ukingoni sasa.

Kati ya timu ambazo ziko kwenye hatari zaidi ni; Dodoma Jiji yenye alama (32), Mtibwa Sugar (31), Ruvu Shooting (28), Tanzania Prisons (26), Biashara United (25) na Mbeya Kwanza ambayo inashikilia nafasi ya mwisho ikiwa na alama (24) pekee baada ya kushuka dimbani mara 28.

Hata hivyo, bado kuna mnyukano mkali kwenye nani anaweza kushuka kutokana na timu zote kukaribiana alama na Magoli ya kufunga na kufungwa; Dodoma Jiji inamagoli ya kufunga 24 ikifungwa 35 (-11), Mtibwa Sugar amefunga 23 akifungwa 27 (-4), Ruvu Shooting inamagoli ya kufunga 25 ikifungwa 38 (-13), Tanzania Prisons yenyewe imefunga magoli 20 ikifungwa 33 (-13), Biashara United nayo inamagoli ya kufunga 21 huku ikifungwa magoli 31 (-10) wakati Mbeya Kwanza wao wakiwa na magoli 21 ya kufunga na wakiruhusu mabao 37 hivyo kudaiwa jumla ya magoli 16 sawa na kuandika (-16).

Ushindani mwingine uliopo katika Ligi Kuu ya NBC msimu huu 2021/2022 unaomalizika Juni, ni kuhusu nani atachukua kiatu cha ufungaji bora, kutokana na mtifuano unaoendelea ukiwahusisha washambuliaji wawili Mzawa George Mpole na Mgeni Fiston Mayele ambao wote mpaka sasa(28) wamefunga magoli 16 kila mmoja. Tofauti iliyopo kwao ni kwenye mchango wa magoli yaani (‘Asissts’) Mpole ana 3 wakati Mayele ana 5; hivyo, hadi sasa Mpole kauhusika kwenye magoli 19 wakati Mayele akiwa kahusika kwenye mabao 21. Kwa hiyo bado vitendawili viwili vinaendelea; timu zinazoshuka na mfungaji bora.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.