Mechi za play off kati ya Pamba SC na Kagera Sugar FC, na Geita Gold FC na Mwadui FC zilizokuwa zichezwe leo ( Juni 2) zimesogezwa mbele hadi kesho ( Juni 3 ) kutokana na sababu za kiusalama.

Mechi zote, zikiwemo za marudiano zitakazochezwa Juni 8 zitaoneshwa moja kwa moja ( live ) na kituo cha televisheni cha Azam TV.

Usalama wa magari ya Azam TV ulikuwa mdogo kutokana na baadhi ya washabiki kutishia kuvunja vioo wakipinga mechi hizo kuoneshwa.

Kwa mujibu wa Kanuni za Ligi, haki za matangazo ya televisheni ni mali ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Timu itakayozuia mechi yake kuoneshwa, itahesabika kuwa haikufika uwanjani, hivyo itachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni.

Viongozi wa timu husika waepuke kutoa matamko ambayo ni kinyume na kanuni za mpira wa miguu. Kwa watakaokwenda kinyume watachukuliwa hatua za kinidhamu na kimaadili.