Ligi ya mabingwa wa mikoa (RCL) 2021 imeendelea kwa michezo miwili kuchezwa kwenye uwanja wa Ilulu, Lindi.
Mchezo wa kwanza uliochezwa saa 8 mchana TMA Stars ya Arusha walicheza dhidi ya Copco Veterans ya Mwanza, mchezo ambao ulimalizika kwa TMA Stars kupata ushindi wa mabao 2-1.yalipachikwa kimiani na Beni Raphael dakika ya 32 na Omary Matwiko dakika ya 86 lile la Copco Veterans likifungwa na Zacharia Paschal dakika ya 82.
Mchezo wa pili uliochezwa saa 10 jioni wenyeji Lindi United walikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Temeke Squad bao likifungwa na Idrisa Khatibu dakika ya 44 kipindi cha kwanza.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa Nyaishozi SC ya Kagera kucheza na Baga Friends ya Pwani saa 10 jioni kwenye Uwanja huo huo wa Ilulu.