Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo limezindua jezi mpya ya timu za Taifa zitakazotumika nyumbani na ugenini.

Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo alikua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars Paul Makonda.

Jezi zilizozinduliwa zimebeba rangi halisi za bendera ya Tanzania.

Zitaanza kutumika rasmi Kesho wakati Taifa Stars itakapokua kibaruani kucheza dhidi ya Misri katika mchezo wa kirafiki utakaochezwa mji wa Alexadria,Misri.

Taifa Stars inajiandaa na mashindano ya AFCON yanayotarajia kuanza Juni 21,2019 na imepiga Kambi nchini Misri.