Mtibwa Mambo Safi, Prisons Hoi Simba Namungo Rekodi Ile ile
Michezo mitatu ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara iliendelea kurindima Novemba 16, 2022 katika viwanja vitatu tofauti na kumalizika kwa timu ya Mtibwa kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union ya Tanga, Simba nayo ikiendeleza ubabe wake mbele ya Namungo huku Tanzania Prisons yenyewe ikiduwazwa nyumbani baada ya kupokea kipigo cha 4-2 kutoka kwa kwa Geita Gold.
Mchezo wa kwanza uliopigwa katika uwanja wa Manungu Turiani Morogoro majira ya saa 8:00 mchana, wa pili ukawakutanisha Tanzania Prisons dhidi ya Geita Gold ukipigwa majira ya saa 10:00 jioni kwenye dimba la Sokoine Mbeya huku ule wa mwisho ukiwakutanisha kati ya Simba na Namungo FC kwa Mkapa jijini Dar es Salaam, saa 1:00 usiku.
Michezo yote ili malizika kwa timu moja kulala dhidi ya nyingine; wafungaji wa magoli kwa Mtibwa walikuwa ni Onesmo Mayaya dakika ya 2 na Juma Nyangi aliyefunga mnamo dakika ya 32 huku goli pekee la Coastal Union likfungwa Moubarack Amza kunako dakika ya 13 ya mchezo huo.
Katika mchezo wa pili goli la kufungua mlango kwa wenyeji Tanzania Prisons lilifungwa na Oscar Paul dakika ya 11, Yusuph Kagoma akaisawazishia Geita Gold mnamo dakika ya 33. Mnamo dakika ya 45 kipindi cha kwanza Danny Lyanga alitanguliza Geita kwa kufunga goli la pili.
Mara tu baada ya timu kurejea kwenye kipindi cha pili Tanzania Prisons wakafanikiwa kusawazisha bao la pili dakika ya 46, kupitia kwa Shwaan Oudoro (own goal); kunako dakika ya 58 Geita nao wakapata bao la tatu kupitia kwa Shwaan Oudoro kisha baadaye Edmundi John akakomelea msumari wa nne na kuifanya Prisons kupata kipigo kikubwa katika uwanja wa nyumbani.
Kwa upande wa Simba na Namungo, mfungaji alikuwa Moses Phiri akitupia kunako dakika ya 31 ya mchezo baada ya kusaka mabao kwa dakika 30 za kipindi cha kwanza. Matokeo hayo yanaifanya Simba kufikisha alama 24 na kuindoa Young Africans iliyokuwa ikishikilia na nadasi ya pili ikiwa na alama 23 huku ikiwa na michezo kadhaa mkono.