Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti Ndairagije Ettiene amempumzisha Nahodha Mbwana Samatta kutoka katika Kikosi alichokitaja kitakachojiandaa na mchezo wa Kirafiki dhidi ya Sudan.

Ndairagije amesema amewasiliana na Samatta ambaye ameomba mapumziko kwakuwa hayuko sawa kwa asilimia 100 kufuatia maumivu ya Goti aliyoyapata kwenye mchezo dhidi ya Burundi.

Amesema nafasi hiyo amemuongeza Mshambuliaji Ditram Nchimbi ambaye pia anaweza kutumika kwenye mchezo wa marudiano wa CHAN dhidi ya Sudan utakaochezwa Oktoba 18,2019 nchini Sudan.

Kikosi kitaingia Kambini Jumapili Oktoba 6,2019 kujiandaa na mchezo wa Kirafiki dhidi ya Rwanda utakaotumika kama sehemu ya maandalizi ya CHAN.

Mchezo huo wa Kirafiki dhidi ya Rwanda utachezwa Kigali Oktoba 14,2019.