Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeingia mkataba wa mwaka mmoja na Ndayiragije Ettiene kuwa Kocha Mkuu wa Taifa Stars.
Kabla ya uteuzi huo uliofanywa na Kamati ya Utendaji ya TFF, Ndayiragije alikuwa Kocha wa muda wa Taifa Stars.
Uamuzi wa Kamati ya Utendaji kumpa Ndayiragije nafasi hiyo ulizingatia mapendekezo ya Kamati ya Ufundi ya TFF ambayo ilipitia wasifu wa makocha mbalimbali walioomba nafasi hiyo.
Wakati akikaimu nafasi hiyo, Ndayiragije raia wa Burundi aliiwezesha Taifa Stars kufuzu kucheza fainali za CHAN zitakazofanyika mwakani nchini Cameroon
Pia aliiwezesha Taifa Stars kuingia hatua ya makundi ya mechi za mchujo za Kombe la Dunia