Nyaishozi yaichapa Black Stars

Timu ya Nyaishozi ya Kagera imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Black Stars ya Tabora katika mchezo wa Fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa uliochezwa Uwanja wa Ilulu, Lindi.

Mabao hayo yalipatikana katika dakika ya 10 na 64 kupitia kwa Idrisa Stambuli.

Baada ya mchezo huo Kocha wa Nyaishozi Karim Amri, amesema Wachezaji wake walijituma na kufuata maelekezo aliyowapa.

Amesema wamepoteza nafasi kadhaa katika mchezo huo kutokana na kukosa umakini katika eneo la ushambuliaji jambo ambalo atalifanyia kazi kabla ya mchezo unaofuata.

Kocha wa Black Stars Elisha Emanuel amesema watafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo wa leo

Fainali hizo za RCL zitaendelea kesho kwa michezo miwili Temeke Squad watacheza dhidi ya TMA Stars saa 8 mchana wakati Copco Veterans watacheza na wenyeji Lindi United saa 10 jioni.

Michezo hiyo itaruka Mbashara kipitia TFF Tv na Radio mtandao ya TFF.