Timu za Pan African FC ya Dar es Salaam na Mbuni FC ya Arusha zimetoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa Fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa inayoendelea Bariadi,Simiyu
Mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Halmashauri Bariadi, ulianza saa 10 jioni.
Ayoub Ayoub katika dakika ya 17 aliiandikia Pan African bao la kuongoza kabla ya dakika ya 45 kuingo mshambuliaji wa Mbuni FC, Wiston Kasimbazi kusawazisha matokeo yaliyosimama mpaka timu hizo zilipokwenda mapumziko
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kubwa huku kila timu ikitafuta bao na dakika ya 72 mchezaji aliyetokea benchi, Edward Mwaikuju aliipatia bao la pili Mbuni FC.
Mbuni FC wakiwa na imani kubwa ya kuondoka na ushindi katika dakika ya 82 Laurent Mugira alifuta ndoto hizo kwa Mbuni FC baada ya kukwamisha kimiani mkwaju wa penati ambayo ilitokana na mchezaji wa Mbuni FC Edwin Agustino kuunawa mpira kwenye eneo la hatari
Tukio hilo hilo lilimfanya Mwaamuzi Hassani Muhina toka Tanga kumpatia kadi ya njano ya pili iliyofuatiwa na kadi nyekundu.
Fainali hizo zinaendelea kwa michezo miwili itakayochezwa tarehe 12 Mei,2019 katika Uwanja wa Halmashauri.