Fainali za Ligi ya Mabingwa wa Mikoa RCL,leo imepigwa nusu fainali kwenye Uwanja wa Halmashauri Bariadi, Isanga Rangers FC ya Mbeya ikipogea kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Pan African FC ya Dar es Salaam na nusu fainali ya pili ikishuhudia DTB FC ya Dar es Salaam ikipata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mbuni FC ya Arusha.
Mchezo wa kwanza ulisimamiwa na Kamishna Judith Gamba wa Dodoma, Muamuzi wa katikati Abel William wa Morogoro, Muamuzi msaidizi namba moja Ramadhani Kiloko wa Tanga, Muamuzi msaidizi namba mbili Mohammed Msengi wa Pwani na Muamuzi wa akiba Ahmed Arajiga wa Manyara.
Mabao ya Pan Africans kwenye mchezo huo yalifungwa na Abdul Kumbilwa dakika ya 2 na Hamza Nganga dakika ya 69.
Mchezo wa pili ulisimamiwa ma Kamishna, Judith Gamba wa Dodoma, Muamuzi wa katikati Ally Mnyupe wa Morogoro, Muamuzi msaidizi namba moja Gidion Nyansio wa Katavi, Muamuzi msaidizi namba mbili Sikudhani Mkulungwa wa Njombe na Muamuzi wa akiba Hassan Muhina wa Tanga
Kwenye mchezo huo mabao ya DTB yalifungwa na Shomary Khalfan Dakika ya 20,Robert Kobelo dakika ya 32 na Haddo Akida dakika ya 34 wakati mabao ya Mbuni FC yakifungwa na Kelvin Kipokola dakika ya 24 na Abdul Haroun.
Kwa matokeo hayo timu za DTB FC na Pan African FC zitacheza hatua ya fainali Jumapili saa 10 jioni, huku Isanga Rangers FC na Mbuni FC wakipambana kutafuta mshindi wa tatu Jumapili saa 8 mchana, Uwanja wa Halmashauri Bariadi
Mshindi wa kwanza, wa pili na wa tatu watapanda Ligi Daraja la Pili 2019/2020.