Katika mwendelezo wa michezo ya Fainali za Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inayoendela mkoani Simiyu, leo wakazi wa Bariadi wameshuhudi michezo miwili katika uwanja wa Halmashauri Bariadi, kati ya timu ya Mkurugenzi FC ya Katavi ikishinda bao 1-0 dhidi ya timu kongwe ya Pan African FC toka Jijini Dar es Salaam mchezo ulioanza saa 8 mchana.

Mchezo huo ulisimamiwa na Kamishna, Ibrahim Kidiwa kutoka Tanga, Muamuzi wa katikati Ally Mkongwe kutoka Mtwara, Muamuzi msaidizi namba moja Sadi Salum wa Dodoma, Muamuzi msaidizi namba mbili Sikudhani Mkurungwa wa Njombe na Muamuzi wa akiba Ally Mnyupe kutoka Morogoro.

Nahodha Titus Siame wa Mkurugenzi FC katika dakika ya 58 aliiandikia timu yake Goli la kwanza, ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huu

Mchezo wa pili ulioanza saa 10 jioni kati ya Mji Mpwapwa FC na Mbuni FC,ulisimamiwa na Kamishna Judith Gamba kutoka Dodoma, Muamuzi wa katikati Ramadhani Kayoko wa Dar es Salaam, Muamuzi msaidizi namba moja Neema Mwambashi wa Dar es Salaam, Muamuzi msaidizi namba mbili Ramadhani Kiloko wa Tanga na Muamuzi wa akiba Hassan Mhina wa Tanga

Ally Sonda alipachika bao pekee la Mbuni FC dakika ya 90 baada ya piga nikupige langoni mwa Mji Mpwapwa na mchezo kumaliza kwa Mji Mpwapwa kukubali kipigo kutoka kwa Mbuni FC

Kesho fainali hizo zinaendelea kwa michezo miwili, itakayochezwa katika viwanja viwili tofauti katika muda mmoja, Uwanja wa Halmashauri na Uwanja wa shule ya Sekondari ya Bariadi