Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) na Bodi ya Ligi (TPLB) wametoa tahadhari kuelekea mechi za mwisho wa msimu Ligi Kuu Tanzania Bara zinazochezwa kesho kwenye Viwanja tofauti.

TFF na TPLB zimepeleka watu katika michezo hiyo na hatua kali zitachukuliwa kwa wote watakaojihusisha na upangaji wa matokeo.

Tayari TFF na TPLB zimewasiliana na vyombo mbalimbali kwa ajili ya kuchukua hatua kwa viashiria vyovyote vyenye nia ovu.

Viongozi,wadau na wanafamilia ya Mpira wa Miguu wametakiwa kutojihusisha na aina yoyote ya upangaji wa matokeo.

Ligi Kuu ya Tanzania Bara inatarajia kukamilika kesho ambapo hafla ya kukabidhi Kombe la Ubingwa kwa Simba itafanyika Uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo mgeni rasmi atakua Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola.