Pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2019/2020 linafunguliwa rasmi leo kwa michezo mitano kuchezwa kwenye Viwanja tofauti.

Namungo FC wataanza kibarua cha mchezo wao wa Kwanza wa Ligi Kuu wakiwa nyumbani Uwanja wa Majaliwa kuwakaribisha Ndanda,wakati Polisi Tanzania wenyewe wataonja ladha ya Ligi Kuu wakiwakaribisha Coastal Union ya Tanga kwenye Uwanja wa Ushirika Moshi.

Michezo mingine inayochezwa leo Mbeya City watacheza dhidi ya Tanzania Prisons wote kutoka Mbeya,Mbeya City akiwa mwenyeji wa mchezo huo utakaochezwa Uwanja wa Sokoine,wakati Mbao FC na Alliance zote za Mwanza watapigania alama 3 Uwanja wa CCM Kirumba,Mbao akiwa mwenyeji.

Huko Uwanja wa Karume,Musoma Biashara United ya Mara watawakaribisha Kagera Sugar.

Mechi zote zitaanza saa 10:00 jioni