Pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) msimu wa 2019/2020 limefunguliwa rasmi leo kwa michezo mitano kuchezwa kwenye Viwanja tofauti.

Namungo FC wameanza kibarua cha mchezo wao wa Kwanza wa Ligi Kuu wakipata ushindi wa nyumbani wa mabao 2-1 dhidi ya Ndanda kwenye Uwanja wa Majaliwa.

Polisi Tanzania waliwakaribisha Coastal Union ya Tanga kwenye Uwanja wa Ushirika Moshi na Polisi kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Michezo mingine iliyochezwa leo Mbeya City wametoka suluhu 0-0 dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine,wakati Mbao FC na Alliance zote za Mwanza wakigawana alama kwa kutoka sareya was kufungana bao 1-1 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,Mbao akiwa mwenyeji.

Huko Uwanja wa Karume,Musoma Biashara United ya Mara wamekubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Kagera Sugar.

VPL itaendelea kesho kwa Mwadui kuwakaribisha Singida United Uwanja wa Kambarage Shinyanga na Lipuli watawakaribisha Mtibwa Sugar Uwanja wa Samora,Iringa