Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limepokea msaada wa mipira 100 kutoka kwa Mjumbe wa Bodi ya Ligi Azim Khan itakayogawanywa kwa timu za Ligi Daraja la Kwanza na Daraja la Pili.

Akipokea msaada huo,Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amempongeza Khan kwa kuzisaidia timu hizo msaada ambao angeweza kupeleka kwenye timu yake lakini akaamua kutoa kwa wengine.

Amewaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia katika Ligi Daraja la Kwanza na Daraja la Pili ili kuendelea kukuza kiwango cha soka nchini.

“Nianze kwa kumshukuru sana ndugu yetu Azim Khan kwa moyo aliouonesha kwetu na kwa kuguswa na kuona kuwa ipo haja ya kuzisaidia timu zetu zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza na Daraja la Pili hapa nchini ili nazo ziweze kukua na kuendelea kunufaika zaidi.” amesema Rais Karia..

Naye Azim Khan amesema kuna haja ya kupeleka nguvu katika Ligi Daraja la Kwanza na Daraja la Pili ili kuweza kuzijengea mazingira mazuri.

Makamu wa Pili wa Rais TFF Steven Mnguto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi akimkaribisha Rais Karia amesema ni jambo kubwa ambalo limefanywa na Khan kutazama Klabu za Ligi Daraja la Kwanza na Daraja la Pili.

Kila Klabu itapata mipira miwili katika mgawanyo