Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia kwa niaba ya TFF anampongeza Brigedia Jenerali Charles Mbuge Kwa kuteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Joseph Magufuli kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) akichukua nafasi ya Meja Jenerali Martin Busungu ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Akiba.

Amesema Mbuge ni mwanamichezo na mdau mkubwa wa mpira wa miguu ambaye amewahi kuongoza Kamati za TFF na mjumbe wa Bodi ya Ligi.

“Namfahamu Brigedia Jenerali Mbuge katika utendaji wake tokea nikiwa naye kwenye Kamati za TFF na baadaye kwenye harakati za kuanzisha Bodi ya Ligi ambapo alikua ni mmoja wa waliounda Bodi ya kwanza ya Ligi Kuu” amesema Rais Karia.

Ameongeza kua TFF inaamini kuongoza kwake JKT itakuwa chachu ya kukuza zaidi michezo na mpira wa miguu ikizingatiwa timu za JKT Tanzania na JKT Queens zipo chini yake,hivyo zitaendeleza ushindani katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania na Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Premium Lite.

Tunamtakia kila la heri katika majukumu yake mapya,tunamuomba Mungu amuongoze katika utendaji ulio bora.