Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kuwakabidhi TFF hekari 15 za ardhi katika eneo la Kigamboni,Kisarawe 2.

Amesema kwa TFF ni jambo kubwa ambalo linapaswa kupongezwa.

“Hiki kitu ni kikubwa sana na tutalitumia eneo hili kwa lengo lililokusudiwa,kwa niaba ya TFF nampongeza sana mheshimiwa Paul Makonda Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na tunashukuru kwa mchango wake” amesema Rais wa TFF Ndugu Karia

Amesema nia ya TFF ni kuwekeza katika miundo mbinu ya Viwanja ambavyo vitatumika kuzalisha na kuendeleza wachezaji kwa faida ya Taifa.

Ardhi aliyokabidhi leo Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Paul Makonda itasaidia katika msingi wa maendeleo ya Mpira wa Miguu.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.