Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ametuma salamu za pole kwa Ndugu,jamaa,marafiki na Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga kufuatia msiba wa mmoja wa Wafanyakazi wa Clouds Ephraim Kibonde aliyefariki Jijini Mwanza.
Ndugu Karia Rais wa TFF amesema ni mshtuko mkubwa kupokea taarifa za msiba wa Ephraim Kibonde,Kwa niaba ya TFF anamuomba mwenyezi Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi.
“Mwenyezi Mungu awaitie nguvu Familia ya Kibonde,Mkurugenzi wa Clouds Joseph Kusaga,Wafanyakazi wa Clouds,ndugu,jamaa na marafiki,TFF wakati wote wa msiba huu iko pamoja na wafiwa” amesema Rais wa TFF Ndugu Karia.
Enzi za uhai wake marehemu Kibonde alikua mwanafamilia mzuri wa Mpira wa Miguu licha ya kutangaza vipindi vya michezo vya Tv na Radio pia ameshiriki kwenye shughuli mbalimbali za TFF akiwa mshehereshaji (MC).
Mungu ailaze roho ya marehemu Ephraim Kibonde mahala pema peponi,Amina.