Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amewapongeza Viongozi wapya wapya wa Klabu ya Young Africans kwa kuchaguliwa kuiongoza klabu hiyo kwa kipindi cha miaka minne (4).

Rais wa TFF Ndugu Karia amesema TFF itashirikiana na Viongozi hao katika harakati za maendeleo ya Mpira wa Miguu hapa nchini.

Karia amewapongeza Wanachama wa Klabu ya Young Africans kwa utulivu walioonesha katika Uchaguzi huo na kufikia kupata Viongozi wapya watakaowaongoza kwa kipindi cha miaka minne.

Amewataka Wanachama na Viongozi wapya waliochaguliwa katika Klabu hiyo kujikita katika kuiendeleza Klabu ya Young Africans,kuuendeleza Mpira wa Miguu,kuondoa kambi na tofauti zote za Uchaguzi.

Viongozi wapya waliopatikana ni Mwenyekiti Dkt.Mbette Mshindo Msolla,Makamu Mwenyekiti Wilfred Mwakalebela na Wajumbe Hamad Islam,Dominick Ikute,Kamugisha Kalokola,Saad Khimji,Salum Ruvila,Rogers Gumbo,Arafat Haji na Bahati Mwaseba