Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia ana matumaini makubwa kwa timu ya Taifa “Taifa Stars” kufanya vizuri katika mchezo wa marudiano CHAN dhidi ya Sudan utakaochezwa Kesho Ijumaa Oktoba 18,2019 El Merriekh,Omdurman.

Rais Karia amesema licha ya Sudan kupata ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa bado nafasi ya kupata ushindi ugenini ipo.

“Kama wao waliweza kupata goli 1-0 hapa kwetu na sisi bado tunayo nafasi ya kupata ushindi wa zaidi ya goli hilo moja,kikubwa tuiunge mkono timu yetu” amesema Rais Karia.

Ameongeza kuwa huo ni mchezo wa kihistoria baada ya mara kwanza kufuzu CHAN tiketi ilipatikana kupitia mgongo wa Sudan na anaamini wakati huu Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti itafuzu tena kupitia Sudan.

Taifa Stars ipo nchini Sudan ikiendelea kujiandaa kwa mchezo huo utakaochezwa Kesho saa 1 usiku