RCL ni Moto Kilimanjaro
Mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL)ambayo kwa sasa yapo katika hatua za Fainali yamezidi kupamba moto huko Kilimanjaro kutokana na upinzani wa kila timu shiriki kwa namna ambavyo timu hizo zilivyo jiandaa kupambana kwa shauku ya kutwaa ubingwa wa Ligi hiyo na hatimaye kupanda daraja.
Mashindana hayo yanayoendelea wilayani Moshi katika uwanja wa Limpopo TPC yalianza Machi 25, 2022 huku timu zote nane zilizo fuzu kufika katika hatua hiyo ya nane bora zikionekana kuwa na mipango thabiti ya kushinda kila mechi, licha ya kuwa kuna baadhi ya timu kupoteza katika mechi hizo.
Fainali za RCL Kilimanjaro zilianza Machi 25 kwa kupigwa michezo miwili ambapo mchezo wa kwanza ulimalizika kwa Gold City kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Nzega United, huku mechi ya pili TRA akimfunga Stand United bao 1-0. Mechi za Machi 26 Silent Ocean akimshangaza City Gold ya Mbeya kwa kupata alama muhimu baada ya kuifunga mabao 2-0, na mechi ya pili ikimalizika kwa Kasulu United akikubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya TMA Stars.
Mashindano hayo ambayo pia yalihudhuliwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Wallace Karia katika ufunguzi uliofanyika Machi 25, 2022 kwenye uwanja wa Limpopo TPC Moshi aliweza kutoa neon kwa timu shiriki kuwa ni vyema kila timu inayo shiriki mashindano hayo awe ni mwenye kufuata taratibu anazopaswa kufuata kutokana na taratibu za mashindano.
Sambamba na hayo Rais Karia aliwashukuru na kuwapongeza pia TPC kwa ushirikiano, ikiwa ni pamoja na uwanja ambao mechi zote za hatua ya fainali zitacheza michezo yake hapo, huku TPC hao pia wakishirikiana kwa ukaribu na TFF kuwawezesha baadhi ya maofisa katika utendaji wake wa majukumu kwa wakati wote wa mashindani.
Fainali za RCL zinatarajiwa kumalizika mapema mwanzoni wa mezi wa April mwaka huu kwa kuchezwa mcheo wa Fainali kwa timu ambazo zitafanikiwa kufika katika hatua hiyo.