Robo fainali ligi kuu ya vijana U-20 kupigwa julai 13,2022

Robo fainali za ligi kuu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 zitapigwa Julai 13,2022 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam, huku mabigwa watetezi Mtibwa sukari wakianza katika mchezo wa mapema dhidi ya Geita Gold FC majira ya 8:00 mchana.

Michezo mingine ya robo fainali itazikutanisha timu ya Simba sc  dhidi ya wagosi wa kaya Costal Union ikufuatiwa na Azam FC  ambaye anakwenda kujiuliza mbele ya Polisi Tanzania. Kocha mkuu wa polisi Tanzania Omary Bakari amesema kwamba anatambua Azam Fc ni timu bora na wao wamejiandaa vema kuwakabili ili waweze kutinga hatua ya nusu fainali na ubora wa Azam hauwapi presha bali unawapa chachu ya kupambana zaidi baada ya kurekebisha makosa yaliyojitokeza kwenye mechi tatu za mwanzo. Naye kocha wa Azam Jonatas Matambala alisema amewaaona  polisi TZ wakicheza  hivyo hana wasiwasi na anaamini atapata ushindi.

Mchezo wa mwisho katika hatua ya robo fainali utakuwa kati ya wanajangwani Young Africans dhidi ya Mbeya kwanza, Yanga akiingia kwa kujiamini zaidi baada ya ushindi wa mchezo wake wa mwisho katika  hatua za makundi wa goli 4-3 dhidi ya Kagera Sugar huku Mbeya kwanza yeye akiingia dimbani akiwa na kumbukumbu ya kutoa sare ya goli 1-1 na Mtibwa sugar.

Kocha wa Young Africans Said Maulidi “alisema haikuwa rahisi kuingia katika hatua ya robo fainali na timu zote zilizotinga hatua hiyo ni timu bora, mchezo utakuwa mgumu lakini nawaahidi mashabiki kwamba nitawapa furaha kwakuwa Yanga hainaga jambo dogo, nawaomba mashabiki mfike kwa wingi uwanjani kuitazama timu yenu”. Wakati kwa upande wa kocha wa Mbeya kwanza Baraka Kibanga alisema wako tayari kapambana ili waweze kuendelea katika hatua inayofuata licha ya ushindani mkubwa ambao umeonekana tangu kuanza kwa ligi hiyo.

Ligi kuu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ilianza kurindima Julai 5, 2022 na inatarajiwa kumalizika Julai 17,2022.