Robo Fainali Ngoma Ngumu WRCL

Ligi ya Mabingwa wa Mkoa kwa Wanawake 2023 inatarajia kuendelea kwa kupigwa michezo ya robo fainali Julai 23, 2023 kwenye uwanja wa Nyamagana.

Hatua hiyo imefikia baada ya mechi za hatua ya makundi kumalizika ambapo timu 8 pekee zilizofanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali, huku nyingine 11 zikishindwa kuendelea mbele.

Timu zilizotinga hatua ya robo fainali ni Mpaju Queens, Njombe FDC Queens, Mwanga City Queens, Ziba Sekondari, Gets Programm, Mara Princess Sayari Woman na Ifakara Home Queens.

Mechi zote za hatua hiyo zitachezwa kwenye uwanja wa Nyamagana kuanzia majira ya saa 2:00 asubuhi na mechi ya mwisho ni saa 10:00 jioni.

Akizungumza kuelekea mchezo huo meneja mashindano wa TFF Baraka Kizuguto alisema maandalizi yamekamilika na kwamba kila kitu kiko sawa, huku akiwaomba wakazi wa maeneo jirani kuendelea kujitokeza uwanjani ikiwa ni sehemu ya hamasa na kuunga mkono kinachofanywa na TFF katika kukuza soka la wanawake.