Nahodha wa Timu ya Taifa “Taifa Stars” Mbwana Samatta anatarajia kutua usiku kujiunga na Kambi ya Kikosi hicho iliyoanza Jumamosi kujiandaa na mchezo wa kufuzu AFCON 2021 dhidi ya Equatorial Guinea Ijumaa Novemba 15 Uwanja wa Taifa.

Samatta anayecheza KRC Genk ya Belgium anatarajia kuiongoza Taifa Stars kwa mchezo huo dhidi ya Equatorial Guinea na mchezo utakaofuata siku 4 baadaye dhidi ya Libya utakaochezwa ugenini.

Wachezaji wengine wanaocheza nje ya Tanzania wanaotarajia kuwasili leo usiku ni Farid Mussa anayecheza Tenerife ya Hispania na Simon Msuva anayecheza Difaa El Jadid ya Morocco.

Wachezaji wanaocheza nje ya Tanzania ambao tayari wameripoti Kambini ni David Kisu(Gor Mahia,Kenya),Ramadhan Kessy (Nkana,Zambia) na Eliuter Mpepo (Buildcon,Zambia)

Taifa Stars tayari imeanza mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa ikipiga Kambi kwenye Hoteli ya Blue Saphire,barabara ya Pugu.

Mchezo dhidi ya Equatorial Guinea utachezwa saa 1 usiku Uwanja wa Taifa Ijumaa Novemba 15.

Kiingilio kwenye mchezo huo ni shilingi 3,000 mzunguko,5,000 VIP B na C