Semina ya kuwajengea uwezo waamuzi wa Wanawake imefungwa leo Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya TFF ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Kagera Saloum Chama akizungumza wakati wa ufungaji wa semina hiyo amesema Muamuzi mzuri ni yule anayezingatia nidhamu,Maadili na mazoezi.
Amesema kama Muamuzi hazingatii mambo hayo ni ngumu kuweza kusogea katika kuchezesha kwenye ngazi za juu.
Ameongeza kua Waamuzi wa Kike watakaofanya juhudi watasaidiwa kufikia lengo.
Waamuzi 35 kutoka mikoa mbalimbali wameshiriki katika semina hiyo ya siku 4 iliyofanyika Makao Makuu ya TFF,Karume Ilala.
Huu ni muendelezo wa semina mbalimbali zinazofanywa na TFF za kujenga uwezo ikiwa tayari zimefanyika semina kwa viongozi wa Klabu za Ligi Kuu ya Wanawake na Semina ya Makatibu wa Vyama vya Mpira wa Miguu vya Mikoa.