Semina ya waamuzi yahitimishwa TFF

Makamu wa pili wa Rais wa TFF Steven Mnguto amehitimisha rasmi semina ya siku tano ya waamuzi wa FIFA na Elite leo Novemba 25, 2022 katika makao makuu ya TFF Ilala, Dar es salaam

Semina hiyo imelenga kupitia na kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza katika michezo ya ligi iliyopita ili yasijirudie katika michezo ijayo na kutimiza matakwa ya FIFA ya kufanya tathimini kwa waamuzi kila baada ya miezi mitatu na matokeo ya tathimini hiyo kutumwa FIFA.

Akizungumza wakati wa kufunga semina hiyo Steven Mnguto alisema kuimarika kwa ligi zetu kunategemea sana weledi wa waamuzi na usahihi wa kutafsiri sheria 17 za mpira wa miguu uwanjani hivyo waamuzi mjipime katika hilo na kila mmoja akatimize wajibu wake”.

Waamuzi 33 kutoka Tanzania bara na visiwani wameshiriki semina hiyo chini ya wakufunzi Leslie Liunda na Israel Nkongo.

Waamuzi walioshiriki ni Amina Kyando, Leonard Mkumbo, Hellen Mduma, Janeth Balama, Jonesia Rukyaa, Ferdinard Chacha, Soud Lila, Florentina Chief, Abdallah Mwinyimkuu, Ally Rajab, Sikudhani Mkurungwa, Ali Mbwana, Ahmed Arajiga, Black Tubuke, Ester Adalbert.

Wengine ni Yusuph Shombe, Handan Said, Raphael Ikambi, Kassim Mpanga, Hery Sasii, Mohamed Simba, Glory Tesha, hance Mabena, Sharif Haji, Nasir Siyah, Joachim Akamba, Tatu Malogo, Hamad Rahid, Gilbert Mrina Frank Komba na Mohamed Mkono.