Serengeti Girls yaingia Kambini kujiandaa na mchezo wa kufuzu kombe la Dunia hey

Timu ya Taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Girls) imeingia  kambini Januari 23, 2024  kujiandaa na mchezo wa hatua ya kwanza wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Zambia.

Timu hiyo iliyoshiriki Fainali za Kombe  la Dunia mwaka 2022 nchini India na kufanikiwa kufika hatua ya robo fainali,  itatupa karata yake ya kwanza kuisaka tiketi ya kufuzu kombe la dunia kwa mara ya pili Februari 03, 2024 ikianzia ugenini. Mchezo wa marudiano utachezwa Februari 11, 2024  katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Kocha Mkuu wa timu ya ‘Serengeti Girls’ Bakari Shime ametaja kikosi cha wachezaji 25 Kitakachoingia kambini kujinoa dhidi ya Zambia.

Wachezaji walioitwa ni; Mariam shabani (Bunda Queens), Mwanaid Maulid (Huru), Salome Saint (Geita Gold Queens), Sarah Joel (Fountain Gate Princess), Edna Edson (Oysterbay Queens), Lidya Maximilian  (JKT Queens), Mikaela Daffa (Geita Gold Queens), Masika Mwakisua (Yanga Princess), Sarah Lucas (Bunda Queens), Kurwa Rocket (Bunda Queens), Manka Richard (Fountain Gate Princess) na Neema Damas (Baobab Queens).

Wengine ni Winifrida John ( Yanga Princess), Ester Maseke (Bunda Queens), Melikia william (Bunda Queens), Naomi Charles (Geita Gold Queens), Asha Omar Ramadhan (Geita Gold Queens), Marry Siyame (Laliga Academy -Spain), Semeni Juma ( Bunda Queens) Sabina Alex (Geita Gold Queens) , Jamila Rajab ( JKT Queens), Yasinta Mitoga (JKT Queens), Mwatima Mwarabu ( JKT Queens ),  Winifrida Gerald JKT Queens) pamoja na Jamila Celestine kutoka timu ya Bunda Queens.

Fainali za Kombe la Dunia zitafanyika katika nchi ya Jamhuri ya Dominika ( Dominican Republic) kuanzia Oktoba 16 hadi Novemba 3 mwaka huu.