Serengeti Girls Yaingia Kambini Visiwani Zanzibar

Kikosi cha timu ya Taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Girls kinachojumuisha takribani wachezaji 32 kimeondoka hii leo Julai 25, 2022 kuelekea visiwani Zanzibar kwaajili ya kujiandaa na maandalizi ya Fainali za Kombe la Dunia 2022 India.

Kocha mkuu wa timu hiyo Bakari Shime amesema kuelekea kwenye Fainali za Kombe la Dunia wameamua kuwa na awamu mbili za kambi kwa ajili ya maandalizi, ambapo timu itaanzia nyumbani Tanzania na awamu inayofuata itakuwa nje ya nchi.

Shime alisema kuwa awamu ya kwanza ya kambi itahusisha wachezaji 32 watakao andaliwa kuiendea michuano hiyo kabla ya mchujo utakao fuatana na maelekezo juu ya idadi ya wachezaji wa na kanuni za michuano hiyo.

Aidha Shime alieleza mipango waliyonayo katika kuiandaa timu kwenye awamu ya pili ya kambi ni pamoja na kuwa na mechi za kirafiki za kimataifa zote zitakazo chezewa huko nje ya nchi ambapo watazingatia timu zenye uwiano na sawa na timu watakazo kutana nazo kwenye hatua ya makundi.

“nimeshazifuatilia timu tulizo pangiwa nazo kwenye kundi letu hivyo lengo letu la kwanza ni kutinga kwenye hatua ya robo fainali, tutawandaa wasichana kimbinu na kisaikolojia kuhakikisha tunafika hapo na endapo tukifanikiwa ndio tutaanza mipango mingine ya kusonga mbele zaidi”. Alisema Shime

Wachezaji walioingia kambini ni; Husna Mtunda( Yanga Princess), Zulfa Makau(Yanga Princess), Anatolia Audax(Mwenge Academy), Neema Majimoto(New Generation), Noela Patrick(Yanga Princess), Christer Bahera(Fountain Gate Princess), Sabituna Salim(JKT Queens), Violeth Nicholaus(Simba Queens), Veronica Gabriel(Mlandizi Queens), Florentina Novatus(Baobab Queens) na Mwamvua Seif.

Wengine ni; Dotto Tossy(Simba Queens), Koku Ally(Simba Queens), Joyce Lema(Fountain Gate Princess), Fatuma Iddy(Amani Queens),Hawa Ally(New Generation), Shehati Juma(Mlandizi Queens), Mwantumu Ramadhani(Baobab Queens),Zawadi Hamis(Fountain Gate Princess), Alia Fikiri(Alliance Girls), Josephine Julius(Baobab Queens),Hasnath Linus(Fountain Gate Princess).

Wachezaji wengine wanaokamilisha idadi ya wachezaji 32 ni; Husna Ayoub(The Tigers Queens), Zainab Mohamed(Baobab Queens), Neema Paul(Fountain Gate Princess), Rahma Salim(Oysterbay Queens), Janeth Cleatus(Amani Queens), Clara Cleatus(Yanga Princess), Diana Mnaly(Fountain Gate Princess), Aisha Juma(Simba Queens), Rehema Mohamed(Mlandizi Queens) na Saida Ayoud(Ruvuma Queens).