Rais Samia : Serikali itatenga fedha kwa Timu za Taifa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaanza kutenga fedha kwaajili ya Timu za Taifa zikiwemo zile za Wanawake.

Akizungumza wakati anahutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Dodoma, Rais Samia amesema, serikali itaanza kutenga fedha kwa ajili ya kuziongezea nguvu timu za Taifa huku akiweka mkazo zaidi kwa upande wa timu za wanawake.

“Tumechoka kuitwa lile jina alilosema mzee Mwinyi (Rais mstaafu awamu ya pili) tunakwenda nje na ushabiki mkubwa tukirudi kichwa cha Mwendawazimu” alisema Rais Samia.

Amesema wataiangalia sekta hiyo ili ipate msukumo na kupandisha ari za Wachezaji ili Tanzania iingie kwenye ramani ya wacheza mpira wa miguu.

Itakumbukwa Rais Samia alikuwa mlezi wa Timu za Taifa za Wanawake kabla ya kumpa jukumu hilo Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Pauline Gekul