Simba Queens Yatangulia Nusu Fainali

Timu ya Simba Queens kutoka Tanzania inayoshiriki kwenye michuano Kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake kanda ya CECAFA tayari imekwisha kujihakikishia kutinga mpaka hatua inayofuata kwenye michuano hiyo mara baada ya ushindi walioupata kwenye mechi zao mbili hatua ya makundi.

Simba Queens imejikatia tiketi hiyo mara baada ya kuichapa timu ya SHE Corporate kutoka nchini Uganda kwa magoli 2-0 kwenye mchezo uliochezwa jumatano Agosti 17, 2022 majira ya saa 8:00 mchana, ikiwa ndio timu pekee kwenye kundi B iliyojihakikishia kwenda hatua inayofuata baada ya kushinda kwenye mechi zake zote mbili .

Mechi ya awali Simba Queens ilipata ushindi wa magoli 6-0 dhidi ya timu ya Y.J.Stars kwenye mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo inayofanyika hapa nchini.

Goli la mapema la Simba Queens limewekwa kambani na mchezaji beki Vivian Aquino Corazone (JN 04)mnamo dakika ya 21 akicheza mpira wa madhambi nje kidogo ya 18 na kumpoteza mlinda mlango Daphine Nyayenga asijue nini cha kufanya.

Kipindi cha pili cha mchezo huo SHE CORP ya Uganda ilijitahidi kupeleka mashambulizi langoni mwa Simba Queens licha ya ugumu wa ukuta huo, hali iliyopelekea SimbaQueens na wao kutengeneza nafasi ya kuandika bao la pili la ushindi lililofungwa namchezaji Pambani Kuzoya( JN 17)mnamo dakika ya 61.

KOcha a Simba Qeens Sebastian Nkoma aliipongeza timu yake kwa kiwango bora walichokionyesha huku akisema bado kuna mapungufu madogo madogomadogo yaliyojitokeza ambayo watakwenda kuyafanyia kazi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufika fainali na kuweza kuwa mwakilishi wa ukanda wa CECAFA katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika kwa wanawake.

Huku kocha wa SHE coparates Charles Lukula akikiri kwamba timu yake imecheza chini ya kiwango katika mchezo wa leo lakini bado wana nafasi moja iliyobaki ya kurekebisha makosa yao na kufanya vizuri katika mchezo wao dhidi ya GRFC utakochezwa siku ya Agosti 20, 2022.