Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Simba Yawaduwaza Al-Ahly kwa Mara Nyingine

Timu ya wekundu wa Msimbazi Simba imefanikiwa kuondoka na alama tatu mbele ya Al-Ahly katika mchezo uliopigwa katika dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliopigwa majira ya saa 10:00 jioni  Simba walionekana kuingia kwa uchu wa kurejea kumbukumbu yao ya kuwafunga A-Ahly  bao moja kwa bila msimu wa 2018-2019 kwenye dimba la Mkapa. Ni dakika 30 tu ziliwatosha Simba kuwa wameandika bao la kuongoza kupitia kwa mchezaji Luis Miquissone; bao lililodumu mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinakamilika.

Kipindi cha pili kilianza huku Al-Ahly wakija na mbinu mpya ya kushambulia ili kuweza kupata bao la kusawazisha. Hata hivyo, Simba walikaa vizuri na kuzidi kujizatiti zaidi ili kuhakikisha lango lao linaendelea kubaki salama.

Makocha wote walifanya mabadiliko kwa kuwatoa wachezaji kadhaa ili kuimarisha vikosi vyao kwa kuwapumzisha wachezaji walioanza ambapo Gomes Da Rosa aliwatoa; Thadeo Lwanga/Erasto Nyoni, Hassan Dilunga/Rally Bwalya, Luis Miquissone/ Francis Kahata, Chriss Mugalu/ Meddie Kagera,  na Kennedy Juma aliyeingia kuchukua nafasi ya Clatous Chota Chama.

Wachezaji walioonesha kiwango bora katika mchezo huo walikuwa ni Luis Miquissone ambaye alikuwa moto mkali ndani ya dakika alizocheza mpaka anaumia huku Joash Onyango naye akionesha umahili wake katika safu ya ulinzi.

Baadhi ya mashabiki wa Simba walisema kuwa kwa Simba hii wanaweza kumfunga Al-Ahly ndani nje na kwamba wanauhakika wa kuingia katika hatua ya robo fainali ya mashindano hayo makubwa kwa ngazi ya klabu barani Afrika.

Kwa kufuatia ushindi huo, Simba sasa wanafikisha alama 6 baada ya kushinda mechi mbili dhidi ya AS Vita ambapo walipata ushindi wa bao moja bila wakiwa nyumbani kwao Congo. Hivyo sasa Simba inaongoza kundi “A” huku AS Vita akiwa wa pili baada ya kupata alama 3 dhidi ya Al-Merrikh ya Sudan, wakati Al-Ahly nao wakishika nafasi ya tatu wakiwa na alama tatu dhidi ya Al-Merrikh ambao ndio wanaburuza mkia kwa kupoteza michezo yote miwili.

Tofauti ya nafasi kati ya AL-Ahly na AS Vita inakuja baada ya AL-Ahly kuruhusu bao moja huku akiwa na magoli 3 aliyoshinda nyumbani kwake dhidi ya El-Merick wakati AS Vita wao wakiruhusu mabao mawili huku wakiwa na faida ya kushinda mabao mengi ugenini baada ya kuifunga Al-Merrikh iliyokuwa nyumbani kwa jumla ya bao 4-1.

Wakati Simba ikifanya hayo kwa Mkapa, Namungo nao wako mguu moja ndani katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuichapa Agosto ya Angola bao 6-2 katika mchezo wao wa awali uliopigwa katika dimba la AZAM Complex Chamazi huku wakisubiri mchezo wa marudiano ambapo Agosto itawabidi kushinda ushindi wa bao zaidi ya 6 au 5 bila, ili kuitoa Namungo.

 

 

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.