Stars “Tuko Tayari Kuitetea Bendera Ya Taifa
Kocaha Mkuu wa kikosi cha Taifa “Taifa Stars” Kim Poulsen amesema kuwa wachezaji wake wako tayari kuendelea kuipeperusha vyema Bendera ya Tiafa la Tanzania kwa kujituma kwa hali na mali kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo wao wa tatu dhidi ya Benin unao tarajiwa kupigwa Oktoba 7, 2021 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Hayo aliyasema Oktoba 06, 2021 wakati akizungumza na waanndishi wa habari za michezo yalipo makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika mkutano uliofanyika majira ya saa saba na nusu mchana (7:30).
Akielezea kuhusu maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo huo, kocha Kim alieleza kuwa wachezaji wake wote wako tayari kisaikolojia, kiakili na kiutimamu wa mwili kwa ajili ya kukabiliana na timu ya Benin na kuhakikisha wanafanikiwa kuibuka na ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri zaidi.
Aidha kocha Kim aliongeza akisema kuwa timu ya Benin ni kati ya timu ngumu na anafahamu fika kuwa mchezo huo wa tarehe 07 Oktoba utakuwa mgumu kutokana na ukweli kwamba timu zote zinaenda kukutana zikiwa na alama sawa (04) huku zikitofautiana kwa magoli ya kufungwa na kufunga.
Kocha huyo alihitimisha kwa kusema pamoja na kuwa timu ya Stars inaongoza kundi bado hiyo haitoshi kuamini kuwa imekwisha kata tiketi ya kufuzu isipokuwa wao kama benchi la ufundi na wachezaji kwa ujumla wanaichukulia kama ni chachu ya kuweza kufanya juhudi zaidi ili kuendelea kuongoza kundi hilo mapka mwisho wa hatua hiyo kwa kuwa lengo ni kufuzu na sio kuongoza tu.
Naye nahodha Msaidizi John Bocco alisema yeye pamoja na wachezaji wenzake wanajua kuwa wanamzigo mkubwa wa kuitetea Bendera ya Taifa kwa hali na mali. Ili hilo liweze timia kazi yao kubwa ni moja tu, kupata matokeo ya ushindi kwenye mchezo huo kabla ya kwenda kurudiana huko Benin Oktoba 10, 2021.
Taifa Stars itashuka dimbani hapo kesho (07 Oktoba, 2021) huku ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mchezo wake dhidi ya Madagascarna nan kutoka sare ya kufungan bao 1-1 na Congo DR; michezo hiyo yote iliyopigwa Septemba, 2021 ambapo mchezo mmoja ulikuwa ugenini huku ule wa pili ukipigwa nyumbani kwenye uwanja wa Mkapa.