Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia ameishukuru Kampuni ya Motisun Group kwa kusaidia Kambi ya ndani ya Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars”.

Akizungumzia msaada huo wa Kambi ya ndani Rais Karia wa TFF amesema ni jambo kubwa limefanywa na Motisun kuiweka Taifa Stars kwenye Hoteli ya Whitesands na kuihudumia kwa siku zote itakazokaa kabla ya kuelekea Misri.

Amesema wakati huu bado TFF haijapokea fedha ya maandalizi kutoka kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika na kuna jitihada nyingine zinafanywa na Serikali kuhakikisha Taifa Stars wanajiandaa vizuri kwa AFCON.

Taifa Stars itaingia Kambini Whitesands kuanzia Juni 1,2019 na itaondoka kwenda Misri Juni 7,2019

Ikiwa Misri Taifa Stars itacheza mchezo wa Kirafiki na Timu ya Taifa ya Misri “The Pharao” Juni 13,2019.

Tayari Kocha Emmanuel Amunike amekwishataja Kikosi kitakachoingia Kambini Juni 1,2019.