Taifa stars kuanza na Morocco AFCON 2024

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kesho Januari 17, 2024  itatupa karata yake ya kwanza kwenye michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) dhidi ya Morocco katika uwanja wa Stade Laurent Pokou, Ivory Coast.

Mchezo huo utachezwa majira ya saa 11 Jioni kwa saa za Afrika Magharibi wakati kwa saa za Afrika Mashariki itakuwa saa 2 Kamili usiku.

Akizungumza na wandishi wa habari kuelekea katika mchezo huo Kocha Mkuu wa Taifa Stars Adel Amrouche alisema, Malengo yake kwa sasa ni kutengeneza timu itakayoweza kushindana katika mashindano ya kimataifa, hasa ukizingatia kwamba Tanzania, Kenya na Uganda ndio nchi zitakazokuwa mwenyeji wa michuano ya AFCON mwaka 2027 hivyo ni lazima tuwe na timu imara itakayoutangaza Ukanda waAfrka Mashariki vizuri.

“Kiujumla kikosi kimejiandaa vizuri kwa mchezo wa kesho na tuna furaha kucheza dhidi ya timu kubwa kwasababu wachezaji watapata nafasi ya kupambnia Taifa na kuonyesha viwango vyao”alisema Amrouche

Naye Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samata alisema “Maandalizi kwa upande wa wachezaji yako vizuri na wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huo

Taifa stars iko katika kundi F pamoja na Morocco, DR Congo na Zambia.