Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” itacheza mchezo wa kirafiki wa Kimataifa na Timu ya Taifa ya Misri Juni 13,2019 Bourg Al Arab,Misri kujiandaa na Fainali za Afrika(Afcon2019)
Mwezi Mei Kocha Mkuu Emmanuel Amunike atataja kikosi kitakachokwenda katika fainali hizowzitakazofanyika nchini Misri
Tanzania ipo kundi C na Timu za Algeria,Senegal na Kenya.
Itaanza kibarua chake kwa kutupa karata dhidi ya Senegal.