Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” leo imeanza mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa,kujiandaa na mashindano ya AFCON yatakayofanyika nchini Misri.

Kikosi hicho kimefanya mazoezi asubuhi wakati kuanzia kesho mazoezi yatafanyika mara mbili kwa siku asubuhi na jioni.

Taifa Stars imeanza Kambi ya ndani iliyopo kwenye Hoteli ya Whitesands kabla ya kuelekea nchini Misri.

Ikiwa Misri Taifa Stars itacheza michezo ya Kirafiki ya Kimataifa na wenyeji Misri Juni 13,2019 na itacheza mchezo mwingine wa Kirafiki Juni 16,2019.

Mashindano ya AFCON yanatarajia kuanza Juni 21,2019,Tanzania ikiwa Kundi moja na Senegal,Algeria na Kenya