Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kimeondoka kuelekea Burundi kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar
Taifa Stars imeondoka na jumla ya wachezaji 23 kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania ATC.
Simon Msuva na Hassan Kessy wanaungana moja kwa moja na Kikosi Burundi
Taifa Stars itatupa karata yake ya kwanza kesho Septemba 4, 2019 kabla ya kurudiana na Burundi Jumapili Septemba 8, 2019 kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar.
Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars Etienne Ndayiragije amesema wanakwenda kwenye mchezo huo wakiwa na lengo moja la kushinda ili kujiwekea nafasi nzuri ya kusonga mbele.
Kwa upande wa Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta amesema amekuja na morali ya ushindi na anaamini watanzani wanafurahia matokeo mazuri dhidi ya Burundi.
Wachezaji wanaounda Kikosi hicho nchini Burundi
Juma Kaseja (KMC)
Metacha Mnata (Young Africans)
Beno Kakolanya (Simba)
Haruna Shamte (Simba SC)
Hassan Kessy (Nkana,ZAMBIA)
Gadiel Michael (Simba)
Mohamed Hussein (Simba)
Kelvin Yondani (Young Africans)
Idd Moby (Polisi Tz)
Erasto Nyoni (Simba)
Jonas Mkude (Simba)
Himid Mao (ENPPI,Misri)
Ally N’ganzi (Minnesota,USA)
Abubakar Salum(Azam FC)
Frank Domayo (Azam FC)
Hassan Dilunga (Simba SC)
Mohamed Issa (Young Africans)
Abdulahziz Makame (Young Africans)
Simon Msuva (Al Jadida,Morocco)
Eliuter Mpepo (Buildcon,Zambia)
Mbwana Samatta (KRC Genk,Belgium)
Abdillahie Yussuf (Blackpool,England)
Farid Mussa (Tenerife,Hispania)
Iddy Nado (Azam FC)
Ayoub Lyanga (Coastal Union)