Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Tanzania Taifa Stars imefanikia kufuzu kushiriki mashinadano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) yatakayo fanyika huko Cameroon 2020
Taifa Stars imefanikiwa kufuzu kwa kuinyuka Sudan bao 2-1 na kufanya matokeo ya jumla kuwa 2-2 na hivyo kuifanya Tanzania kupita kwa kushinda magoli mengi ugenini.

Katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa El Merreck nchini Sudani, timu ya Sudani ilianza kupachika bao lake katika dakika ya 30 kipindi cha kwanza na kuzifanya timu hizo kwenda mapumziko huku Tanzania wakiwa nyuma kwa bao moja.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi zaidi huku Tanzania ikipambana kwa nguvu zaidi kupeleka mashambulizi kwa kasi na kupelekea wapenzani wao Sudani kufanya makosa na hatimaye kuifanyia Taifa Stars kusawazisha goli katika dakika ya 50 kipindi cha pili.
Goli hilo lipachikwa na mchezaji kiraka Erasto Nyoni kwa mpira wa adhabu.

Goli hilo lilipatia nguvu Taifa Stars na kuifanya iongeze bidii zaidi juhudi ambazo zilifanikiwa kuzaa matunda mnamo dakika ya 78 ya mchezo.

Coli is pili la Stars liliongeza hamasa zaidi kwa wachezaji na hivyo kuendeleza mapambano zaidi hatimaye kufanikiwa kulinda ushindi.

Aidha mchezaji Nchimbi aliweza kuwainua mashabiki na wapenzi wengi wa soka na kuifanya Stars iweze songa mbele.
Nchimbi alipachika bao hilo la pili mara baada ya kumalizia crosi iliopigwa Shaban Iddy Chilunda..
naye kupachika bao zuri lililoifanya Stars kuongoza mnamo dakika ya 78 ya mchezo.

Mabadiliko yaliyofanywa na Kocha wa kikosi cha Taifa Stars Ettiene Ndairagije yameonekana kuwa yakiufundi zaidi baada ya kuzaa Matunda nakuifanya Tanzania kuibuka na ushindi ugenini na hivyo kupata fursa ya kushiriki mashindano hayo yatakayo fanyika Cameroon.

Hii ni mara ya kwanza kwa Kocha Ndairagije kupata ushindi akiwa na kikosi cha Taifa ndani ya dakika 90. Ikumbukwe kuwa tangu kocha Ettiene akabidhiwe mikoba ya kukinoa kikosi cha Taifa hakuwahi kupata uahindi ndani ya dakika 90.