Tanzania Kukipiga Robo Fainali na Mwenyeji

Timu ya Taifa ya Tanzania ya wasichana chini ya miaka 12 inatarajia Kukipiga Agosti 22, 2024 kwenye hatua ya robo Fainali dhidi ya mwenyeji wa mashindano hayo ya Female Universal Youth Cup, timu kutokea nchini China “Dingnan”.

Tanzania imefikia hatua hiyo ya robo fainali baada ya kushinda michezo yote mitatu kwenye hatua ya makundi, ambapo mchezo wa kwanza ilifanikiwa kupata ushindi wa magoli 7-0 dhidi ya Indonesia hapo Agosti 20, 2024.

Ikiwa hatua hiyo ya makundi Tanzania iliendelea kugawa dozi ya mabao hata kwenye michezo iliyofuatia, wakati Indonesia akipokea kipigo kizito Cha mabao 10-0, hii Leo Agosti 22, 2024 ilimalizana na timu ya Shantou ya nchini China kwenye mchezo uliomalizika Kwa Tanzania kupata ushindi wa magoli 5-0.

Kwa matokeo hayo, timu ya Taifa ya Tanzania inafanikiwa kusonga mbele zaidi kwenye mashindano hayo ambapo itakwenda kucheza mchezo wa robo fainali na wenyeji Dingnan Agosti 22, 2024.