Tanzania Mwenyeji Integrated Football Tournament (GIFT)

Tanzania imepangwa kuwa mwenyeji mashindano ya kwanza ya CAF ya wasichana U17 ya Integrated Football Tournament (GIFT) yanayotarajia kufanyika kuanzia Januari 7-18, 2025 Dar es salaam, Tanzania.

Mashindano hayo mapya yatakayo zikutanisha timu 8 kutoka Afrika zikitunishiana misuli kwa dhamira ya kuupa nafasi mchezo wa mpira wa miguu kwa mabinti ikiwa ni fursa pia kwa mabinti hao kukuza na kuendeleza talanta zao, yatafanyika kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Timu hizo 8 kutoka ukanda wa Afrika Mashariki( CECAFA) ni pamoja na timu 2 za Tanzania ambazo ni; TDS Girls Academy na timu ya JKT Queens. Timu nyingine ni Aigle Noir FC (Burundi), Bahir Dar Kenema FC (Ethiopia) na Kenya Academy of Sports (Kenya).

Nyingine ni; Boni Consilli Girls Vocational Team (Uganda), City Lights Football Academy (Sudani Kisini) na Hilaad FC (Somalia).

Ikumbukwe hii ni mwendelezo wa kazi kubwa inayofanywa na TFF chini ya uongozi wa Rais Wallace Karia sambamba na juhudi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika CAF katika kukuza vipaji vya mpira wa miguu barani Afrika hususani kwa wanawake.