Timu ya Taifa ya Wanawake U20 “Tanzanite” itacheza na wenyeji Afrika Kusini kwenye mchezo wa nusu fainali ya Mashindano ya COSAFA.

Tanzania imemaliza katika nafasi ya pili kwenye Kundi B baada ya kupoteza mchezo wake wa mwisho wa hatua ya Makundi kwa mabao 2-1 dhidi ya Zambia.

Mchezo wa nusu Fainali utachezwa Alhamis Agosti 8,2019 saa 9 alasiri kwenye Uwanja wa Gelvalande,Port Elizabeth,Afrika Kusini.

Tanzania imekamilisha hatua ya Makundi ikishinda mechi mbili dhidi ya Botswana 2-0 na Eswatini 8-0 kabla ya kupoteza mbele ya Zambia 2-1 na kukusanya alama 6.

Zambia wamemaliza na alama 9 baada ya kushinda michezo yake yote mitatu ya Kundi B wakiifungwa Botswana 4-1,Eswatini 4-0 na Tanzania 2-1.

Katika Kundi A Afrika Kusini wameibuka vinara wakiwa na alama 9,Zimbabwe akimaliza nafasi ya pili na alama 6.

Nusu fainali zote zitachezwa siku moja kwenye Uwanja wa Gelvandale