Kikosi cha Timu ya Taifa ya Wanawake U20 “Tanzanite” leo asubuhi wamefanya mazoezi mazoezi yao ya Kwanza tokea wamewasili Port Elizabeth,Afrika Kusini kwenye mashindano ya Wanawake U20 ya COSAFA yanayoanza leo Agosti 1-11,2019.

Tanzanite itaanza kibarua chake kwa kupambana na Botswana Kesho,mchezo utakaofanyika Uwanja wa Gelvandale.

Kocha Mkuu wa Tanzanite Bakari Shime amesema wanaingia kwenye mchezo huo kwa nia ya kufanya vizuri.

Amesema licha ya hali ya hewa ya baridi iliyopo Port Elizabeth lakini sio kisingizio kwa timu kutofanya vizuri.

Tanzania imepangwa Kundi B na timu za Botswana,Eswatini na Zambia.