Timu ya Taifa ya Wanawawake U20 “Tanzanite” imefanikiwa kutinga Fainali ya COSAFA baada ya kuwachapa wenyeji Afrika Kusini kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Gelvandale,Port Elizabeth,Afrika Kusini.
Mabao ya Tanzania yamewekwa wavuni na Nahodha Enekia Kasonga na Opa Clement.
Mchezo wa Fainali Tanzania watacheza dhidi ya Zambia Jumapili Uwanja wa Wolfson.
Katika mchezo wa nusu fainali Enekia Kasonga ameibuka kuwa mchezaji Bora wa mechi hii ikiwa ni mara ya tatu kwa Tanzania.
Diana Msemwa amechukua tuzo hiyo mara mbili huku Aisha Masaka akiondoka na mpira baada ya kutupia mabao 3 katika mchezo mmoja.
Mpaka sasa katika mashindano hayo Tanzania ndio timu iliyopata ushindi mkubwa zaidi wa mabao 8-0 na ndio timu iliyopata mabao mengi zaidi katika mchezo mmoja,ikimchapa Eswatini kwenye hatua ya makundi.