Tanzania ya Beba Kombe Michuano ya TFF U16,2020
Michuano ya TFF imeendelea hii leo March 14, 2020 kwa kuzikutanisha timu za vijana Tanzania U16 dhidi ya Liberia U16 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Ikiwa ni mchezo wa mwisho mara baada ya timu zote kushinda mchezo mmoja mmoja.
Kwanza kabisa timu hizo zilikutana 10Machi, 2020 ambapo katika mchezo huo Tanzania ilishinda 3-0 na zikarudiana tarehe 12, Mach 2020 Liberia aliibuka na ushindi wa bao 3-1.
Aidha katika mchezo wa leo kipindi cha kwanza timu zote zilionyesha kucheza chini ya kiwango japo mambo yalibadilika katika dakika ya 20 ambapo timu ya Liberia ilijitutumua na kuanza kuandika bao huku Tanzania ikisawazisha katika dakika ya 45 ya kipindi hicho ya kwanza kupitia kwa mchezaji wake Thabit Thabit, jezi namba 03;holi lililozifanya timu hizo zitoke sare ya 1-1 katika 45 za kwanza.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya
mabadiliko ya hapa na pale, ambapo mnamo dakika ya 80 na kitu hivi Liberia wakakomelea msumari wa pili ambapo goli hilo lililodumu kwa takribani dakika 4 tu kabla ya Tanzania kusawazisha goli hilo kupitia mcheza jezi namba 15, Hamis Mohamed na baadaye mupata bao la tatu, kupitia kwa Boniface Nickson Kivelege jezi 07 aliyetokea sub; goli hilo liliifanya Tanzania kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 na hivyo kuwa ndiyo mabingwa wa mashindano hayo ya TFF, 2020.
Kocha wa U16 ya Tanzania Boniface Pawassa amesema alijipanga kushinda licha ya kikosi chake kucheza chini ya mpira katika kipindi cha kwanza na kudai kuwa aliwatega wapinzani wake na wakajikuta wanaingia kwenye mtego ambao timu yake kupata ushindi huo.
Aidha kocha Pawassa ameongeza kuwa mashindano hayo yalikuwa maalum kwa ajili ya kujiandaa kuwapata vijana wa kuunda kikosi cha U17 na U20 Tanzania hapo baadaye.
Kocha wa Liberia Cooper Sannah, yeye amesema kuwa mchezo ulikuwa ni wa ushindani mkubwa na kuongeza kuwa kikosi chake kilionekana kupoteza umakini katika kipindi cha pili na hivyo kupelekea kupoteza mchezo huo ambao alikuwa tayari kishaushika.
Hata hivyo, kocha huyo amesema mashindano hayo yamewapatia wachezaji wake uzoefu mkubwa.
Mabingwa hawa wa timu ya Tanzania walikabidhiwa kombe pamoja na medali na Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania ndugu Wallace Karia, tukio lililoshuhudiwa pia na makamu wa pili wa Rais wa TFF ndugu Steven Mnguto.