Tanzania Yaanza Kwa Ushindi “Female Universal Youth Cup”

Timu ya Taifa ya wasichana U12 inayoshiriki mashindano ya Female Universal Youth Cup Dingnan China imeanza Kwa Miguu wa kulia mashindano hayo baada ya kupata ushindi kwenye mchezo wake wa kwanza.

Mchezo huo uliozikutanisha timu ya Indonesia na Tanzania Agosti 20,2022 ulimalizika kwa Tanzania kupata ushindi wa magoli 7-0, huku wachezaji wawili Ashura Hamad na Debora Joseph wakipachika kimyani magoli mawili mawili kwenye idadi ya magoli yote 7.Magoli mengine yalifungwa na Anna Athanas, Asha Said na Hafsa Said.

Akizungumza baada ya mchezo huo kocha wa timu hiyo Elieneza Nsanganzelu alisema mchezo huo haukuwa rahisi kwao licha ya kupata matokeo mazuri, kutokana na idadi chache ya wachezaji wanaopaswa kucheza kwenye mechi kulingana na Sheria na kanuni za mashindano hayo.

Alisema Kwa muda walionao watakwenda kusahihisha makosa yaliyojotokeza kwenye mchezo huo ikiwa pia ndio sehemu ya kujipanga na maandalizi ya mchezo unaofuata, timu hiyo inatarajia kushuka dimbani Kwa mara nyingine kesho Agosti 21, 2024 dhidi ya City Dream ya nchini humo.

Ikumbukwe Tanzania inashiriki mashindano hayo ikiwa kundi ‘B’ na timu ya City Dream itakayo kutana nayo kesho pamoja na timu nyingine ya nchini humo Shantou Football Association.